11 views 38 secs 0 comments

THE ROYAL TOUR YAZIDI KUIFUNGUA SEKTA YA UTALII.

In BURUDANI
May 09, 2025



Na Mwandishi wetu

Filamu ya The Royal Tour imezidi kuleta matokeo chanya katika sekta ya Utalii kutokana na mwamko mkubwa kwa wawekezaji hususan wa Hotel za kitalii kuendelea kuwekeza kwenye maeneo mbalimbali  hasa kwenye Hifadhi za Taifa ili kwendana na kasi kubwa ya  watalii  wanaoingia nchini.

Akizungumza baada ya kutembelea  Hoteli ya Serengeti Explore by Elewana na Hoteli ya Serengeti Lake Magadi, Mkoani Mara, Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi amesema ujenzi wa Hoteli hizo ni mwitikio wa kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuinua sekta ya Utalii hasa kupitia Filamu ya “Tanzania-The Royal Tour,”  ambayo imechagiza zaidi kuleta wageni wengi  na kufungua fursa zaidi kwa wawekezaji kuwekeza katika malazi.

Aidha Dkt. Abbasi ameendelea kutoa wito kwa wawekezaji kuchangamkia fursa adhimu kuwekeza  kwa kujenga hoteli katika hifadhi za kusini ikiwa ni mkakati wa Serikali katika kuifungua zaidi Kusini pamoja na  kutangaza vivutio vipya vya utalii.

Hoteli ya Serengeti Explore ambayo ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 100 na Lake Magadi ambayo ujenzi wake unaendelea kwa jumla zina vyumba 150, hivyo zinaongeza zaidi wigo wa Hoteli za Kitalii katika kuwahudumia wageni wengi zaidi wanaoingia nchini.

/ Published posts: 2017

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram