UZALISHAJI WA MAZAO ÀSILIA YA BIASHARA YAZIDI KUPAA
JIJINI DODOMA Imeelezwa kuwa uzalishaji wa mazao asilia katika mwaka 2023/2024 umeongezeka kutoka tani 1,123,477.92 mwaka 2022/2023 hadi tani 1,260,321.1 sawa na asilimia 78.05 ya lengo la kuzalisha tani 1,614,758. Hayo yamesemwa na Mhe. Hussein Bashe wakati wa uwasilishaji wa Bajeti ya Wizara ya Kilimo leo Tarehe 02.05/2024 Jijini Dodoma ambapo amesema ongezeko hilo limechangiwa […]