Azam TV vinara wa huduma bora za maudhui na burudani za kusisimua nchini, kwa mara nyingine wanajivunia kutangaza uzinduzi wa tamthilia mbili zilizokuwa zikisubiriwa kwa muda mrefu zinazoitwa ‘Mtaa wa Kazamoyo’ na ‘Lolita’. Tamthilia hizi zilizobeba simulizi za kuvutia si tu kwamba zinakuja kuleta mapinduzi ya tasnia ya tamthilia nchini, bali zinaakisi maisha halisi ya […]
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema taaluma ya Uuguzi ni kazi ya uthubutu, utayari pamoja na kujitoa kwa ajili ya kuwahudumia wenye mahitaji ya kiafya huku akiwataka Wauguzi kuendelea kuchapa kazi kwa weledi na kwa kuzingatia miiko na maadili ya taaluma yao. Mhe. Kikwete […]
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amesema Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia inapaswa kuangazia changamoto zinazowagusa wananchi wa hadhi zote wakiwemo watu wenye ulemavu na wanaofanyiwa ukatili wa kijinsia. Makamu wa Rais amesema hayo leo tarehe 22 Julai 2023 wakati akizindua Kampeni ya […]
Mbunge wa Jimbo la Kibakwe ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene ametoa onyo kwa wananchi wanaoharibu vyanzo vya maji huku akiutaka Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa kusimamia ipasavyo zoezi hilo. Mhe. Simbachawene ametoa agizo hilo wakati akizungumza na wananchi […]
Manchester United wamekamilisha usajili wa mlinda mlango Andre Onana kutoka Inter Milan kwa kima cha pauni milioni 47.2m. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Cameroon mwenye umri wa miaka 27, ametia saini mkataba wa miaka mitano, na chaguo la kuongezwa kwa miezi 12. Mkataba huo una thamani ya pauni milioni 43.8 pamoja na nyongeza zinazoweza kufikia […]
.Zambia, DRC nazo zakimbilia uwekezaji wa UAE WAKATI baadhi ya wanasiasa wa upinzani na wanaharakati wakipinga mpango wa kampuni ya DP World ya Dubai kuwekeza kwenye bandari ya Dar es Salaam, Kenya imetangaza maamuzi ya kusaini mikataba ya uwekezaji na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE). Rais William Ruto ametangaza kupitia akaunti yake ya Twitter […]
Nairobi. Hali ni tete nchini Kenya, huku watu saba wakidaiwa kupigwa risasi wakati wa maandamano yanayoendelea yakiongozwa na Kiongozi wa Upinzani, Raila Odinga. Taarifa zinasema watatu kati ya waliopigwa risasi ni katika Kaunti ya Nakuru, wawili Makueni na wengine wawili Migori. Msimamizi wa hospitali iliyoko Migori, Oruba Ochere alithibitisha kuwa wanaume wawili waliojeruhiwa kwa risasi […]
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene, amewataka wananchi kuibua miradi ya kimkakati katika maeneo yao ili Serikali iweze kusaidia katika ukamilishaji wa miradi hiyo. Ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wananchi kwa nyakati tofauti katika Kata ya Luhundwa, Lufu, Wangi na Wotta, Wilayani Mpwapwa, Mkoani […]
Tanzania imeshiriki Mkutano wa Sita wa Kamati Maalum ya Mawaziri wa Fedha, Mipango ya kiuchumi na Mtamangano wa Afrika, uliobeba kaulimbiu ya “Afrika baada ya Majanga”: Majadiliano juu ya Uwekezaji, Ukuaji Endelevu wa Uchumi na Ustawi kwa wote”. Mkutano huo uliojumuisha nchi 55 wanachama wa Umoja wa Afrika, umefanyika Jijini Nairobi nchini Kenya. Mkutano huo […]
Waziri wa Fedha. Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Mhe. Nicolas Kazadi, kuhusu mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kutoka Uvinza nchini Tanzania hadi Gitega nchini Burundi kupitia Musongati kwenye machimbo ya madini na kipande kingine cha reli kinachokusudiwa kufika […]