WAZIRI MKUU AKAGUA ATHARI ZA MVUA LINDI, ATOA MAELEKEZO KWA MAMENEJA WA TANROADS NCHINI
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameagiza Mameneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) wote nchini kuhakikisha wanakagua vipenyo vya makalvati na madaraja yote katika maeneo yao kabla na baada ya msimu wa mvua ili kujiridhisha kama vinapitisha maji kwa urahisi bila kuathiri barabara. Majaliwa ametoa maelekezo hayo leo Aprili 16, 2025 mara baada ya kuwasili mkoani Lindi […]