DCEA YAKAMATA KILO 4,568 ZA DAWA ZA KULEVYA, yazuia tani 14 za kemikali bashirifu za bangi kuingia nchini, yateketeza ekari 178 za mashamba ya bangi na magari saba
NA MWANDISHI WETU MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), kwa kushirikiana na vyombo mbalimbali vya dola, imefanikiwa kukamata jumla ya kilogramu 4,568 za dawa za kulevya, kuteketeza ekari 178 za mashamba ya bangi na magari saba, pikipiki tano na bajaji moja zimekamatwa kwa kuhusika katika shughuli za usafirishaji wa dawa hizo. […]