45 views 32 secs 0 comments

GAVANA BWANKU ATEMBELEA KUONA NA KUKAGUA BILIONI 1 YA RAIS SAMIA ILIVYOJENGA SHULE YA KISASA YA SEKONDARI KAITORO.

In KITAIFA
April 06, 2025



_Kuanza kupokea Wanafunzi 160 wa kidato cha 5 Julai, ina madarasa 12 ya kisasa, mabweni mawili, nyumba ya Walimu 2 in 1 n.k._

Kata ya Kaitoro kwenye Tarafa ya Katerero ilikua na Sekondari moja lakini kutokana na uwingi mkubwa wa wanafunzi, mwaka juzi 2023 Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan ikaamua kujenga shule nyingine hii kubwa ya kisasa ya Kaitoro.

Afisa Tarafa hii ya Katerero mkoani Kagera Ndugu Bwanku M Bwanku wiki hii ametembelea kuona maendeleo ya shule hiyo na kukagua ujenzi wa mabweni mawili makubwa yanayoendelea kujengwa shuleni hapo ili kupokea wanafunzi wa kidato cha 5 Julai mwaka huu. Pia Afisa Tarafa Bwanku alitembelea madarasa, ofisi za walimu, vyoo na nyumba ya walimu.

Mradi ni mkubwa sana na wa kisasa ukigharimu takribani Bilioni 1 na milioni 65 zilizotolewa na Serikali ya Rais Samia na tayali wanafunzi wa kidato cha kwanza hadi cha nne wanaendelea kupata masomo huku taratibu za kukamilisha ujenzi wa mabweni ukiendelea ili kupokea wanafunzi wa kidato cha 5 mwezi Julai mwaka huu. Afisa Tarafa aliambatana na Mtendaji wa Kata Ndugu Hamza Masudi, Mtendaji wa Kijiji cha Musira shule ilipo Ndugu Wilfred Maganya na Mkuu wa Shule hiyo Julius Kashubao

/ Published posts: 1975

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram