

Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM WAMACHINGA
Waziri kivuli wa Viwanda na Biashara ambaye pia ni Mwanasheria, Katibu wa Mambo ya Nje ACT Wazalendo Mwanaisha Zuberi Mndeme ametia nia ya kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya ubunge katika Jimbo la Kigamboni katika kuelekea kwenye uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025.
Licha ya Chama cha CHADEMA kikiendelea na sera yao ya “No Reform No Election” katika kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 2025 kwa upande wa ACT Wazalendo katika Jimbo la Kigamboni Mwanaisha Mdeme amechukua fomu ya kugombea ubunge huku akihakikisha kuwa sababu kubwa ni kuwapatia wananchi wa Kigamboni kuwa na haki ya kupata kiongozi wanaye mtaka.
Ameyasema hayo Leo 30 April 2025 Katibu wa Idara ya mambo ya nje na waziri kivuli wa Viwanda na biashara wa chama Cha Act WAZALENDO Mwanaisha Mndeme Amesema Wakurugenzi wa halmashauri wasimamie uchaguzi,iteuliwe tume mpya ya uchaguzi,kusiwe na kura feki, vyombo vya Dola vijiepushe na hujuma kwenye uchaguzi na Mawakala wasibughudhiwe na wagombea wasienguliwe
Mndeme Amesema Kupitia taaluma yake ya Sheria ataungana na wabunge wenzake kutunga Sheria zenye tija Kwa wanakigambini na watanzania Kwa ujumla
“Shabaha ya chama chetu ni kuona rasilimali za nchi hii zinamnufaisha kila mtanzania,nitakuwa sehemu ya kutunga Sheria zitakazo Linda rasilimali za nchi yetu”Amesema Mndewe
Mndewe Amesema kigamboni kunachangamoto za Muda mrefu ya miundombinu mibovu ya barabara za Kata tatu ambazo ni Kimbiji,Pembamnazi,Kisarawe ambazo hazina barabara za lami na kupelekea changamoto ya usafiri kwa wanakigamboni
Aidha Mndewe ameiasa serikali kuwa haipaswi kukimbia wajibu wake wa kutoa huduma ya kuvusha wanakigamboni Amesema kigamboni kunavivuko vitatu vya kuvusha wanakigamboni kutoka magogoni mpaka feri na kimebaki kivuko kimoja Cha MV kazi licha ya kazi inayofanywa na bakheresa limited ya kivuko Cha Sea Tax.
Pia Amewataka NSSF watoe taarifa ya lini biashara ya kulipia daraja la Mwalimu Nyerere lini inafika mwisho
Mndeme ametia Nia yake na kusema kuwa atatatua kero zilizopo kigamboni”nitafanya kazi Kwa ukaribu na wananchi,nitasikiliza changamoto zenu na Kwa ushirikiano wa kweli,tutaweka mipango ya haraka,ya kati na ya Muda mrefu kuhakikisha tunaleta mabadiliko yanayoonekana,siyo maneno matupu”Ameongeza Mndewe