Na Happiness Shayo-Dar es Salaam Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) amewataka Watanzania kuwaenzi mashujaa kwa kuendeleza utu, amani na ubinadamu walioupigania ili kuifanya dunia kuwa mahali salama pa kuishi. Ametoa kauli hiyo leo alipokuwa mgeni rasmi katika Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa waliopigania Vita ya Kwanza ya Dunia iliyofanyika […]
Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA Rais Samia apeleka neema Tabora -TABORA WAKALA wa Nishati Vijijini (REA) unatekeleza mradi wa Shilingi Bilioni 19 wa kusambaza umeme katika vitongoji 180 utakaonufaisha kaya 5,940 mkoani Tabora. Hayo yalisemwa jana na Msimamizi wa Miradi ya REA Kanda ya Magharibi, Mhandisi Robert Dulle mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paul […]
Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA Ni wakati akitoa mchango Bungeni kuhusu Mpango wa Taifa wa Maendeleo* Ataja kuongezeka kwa kiasi cha umeme katika Gridi ya Taifa* Aeleza usambazaji umeme vijijini ulivyofanyika kwa mafanikio; Vijiji 78 Tu vyasalia* Aeleza jitihada zilizofanyika Sekta ya Mafuta na Gesi Asilia; Utoaji wa Leseni na Duru ya Tano ya kunadi vitalu* […]
Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA Arusha Ijumaa 8 Novemba 2024 , Tanzania imefanya mkutano muhimu wa Afya Moja jijini Arusha, ukiwaleta pamoja maafisa wa serikali, washirika wa kimataifa, mashirika ya kiraia, na wataalam ili kuendeleza mbinu ya Afya Moja kama mkakati muhimu kwa usalama wa afya duniani na maendeleo endelevu ya binadamu. Tukio hilo la hadhi […]
Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA -DAR ES SALAAM WAZIRI Mkuu Mstaafu, Mzee John Malecela, amesema ziara za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan zimeleta manufaa makubwa ikiwemo kuiweka Tanzania katika sura nzuri kimataifa na kuimarisha ushirikiano. Amesema katika kipindi hiki cha uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia, maendeleo ya kasi yameshuhudhiwa […]
Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA KATIBU wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla, amesema Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitatumia 4R za Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kufanya kampeni za kistaarabu na kuheshimiana katika uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji. Amesisitiza kuwa viongozi na wanachama wa CCM watakaopata fursa […]
Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA Kunufaisha kaya 2,970 kutoka kwenye vitongoji 90 ndaniya wilaya tatu, RC Macha asema umeme ni kipaumbele cha Rais Samia -SHINYANGA SERIKALI kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) inatekeleza mradi wa Shilingi bilioni 11.18 wa kusambaza umeme katika vitongoji 90 utakaonufaisha kaya 2,970 mkoani Shinyanga. Hayo yalisemwa jana na Msimamizi wa Miradi […]
Na Catherine Sungura KIGOMA WAMACHINGA Bajeti ya dharura nayo yaongezezeka Ndani ya kipindi cha miaka mitatu ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, bajeti ya uboreshaji wa miundombinu ya barabara za TARURA imeongezeka kutoka Shilingi Bilioni 275 hadi Shilingi Bilioni 710. Hayo yameelezwa mwishoni […]
Donald Trump ameshinda uchaguzi wa urais nchini Marekani 2024. Trump ameibuka mshindi baada ya kumshinda mpinzani wake kutoka chama cha Democrats bi Kamala Harris. Mgombea huyo wa Republican alipata ushindi mnono dhidi ya Kamala Harris, unaomruhusu kurejea katika kiti cha urais wa Marekani. Trump, ambaye alishinda uchaguzi wa 2016 na kupoteza ule wa 2020, alichukua […]