49 views 55 secs 0 comments

POLISI DAR YAIPIGA MARUFUKU CHADEMA KULETA VURUGU MAHAKAMANI

In KITAIFA
April 17, 2025

Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM WAMACHINGA

Jeshi la polisi kanda maalumu dar es salaam limesema kuwa kuanzia April 18,2025 waumini wa dini ya kikristo wanaanza kuungana na wenzao duniani Kwa kusheherekea sikukuu ya pasaka itakayo sheherekewa Tarehe 20, April 2025 ambayo itahusisha Ibada mbalimbali zitakazo fanyika Katika nyumba za Ibada usiku na mchana

Ameyasema hayo Leo 17 April 2025 Kamanda wa Kanda maalumu ya polisi dar es salaam muliro Jumanne muliro Amesema polisi ya dar es salaam imejipanga vizuri kuhakikisha waumini wanashiriki na kusheherekea sikukuu hiyo Kwa amani na utulivu

Aidha ametoa wito Kwa wazazi na walezi kuwa na uuangalizi wa karibu Kwa watoto wakati wa matembezi na makusanyiko mbalimbali na usalama wa barabarani limesisitizwa Kwa madereva Kwa kuzingatia Sheria za barabarani kuepusha ajali.

Pia muliro Amesema ikifuatia matamko mbalimbali na mipango ya baadhi ya viongozi wa chadema kuhamasisha watu kukusanyika Tarehe 24 April 2025 Katika eneo la mahakama ya kisutu Kwa kutaka kufanya vurugu Kwa lengo la kushinikiza mamlaka za kisheria kumwachia mmoja wa mtuhumiwa Tundu lissu atakayepelekwa siku hiyo mahakamani

“Jeshi la polisi kanda maalumu dar es salaam linawakumbusha wahusika kuwa mahakama ni mamlaka za kisheria zilizo huru na hazipaswi kutishwa au kuingiliwa”. Amesema Muliro

Muliro Amesema jeshi la.polisi linawatahadharisha watu wote wanaohamasisha kuhusiana na Nia hiyo ovu kutoshiriki kwenye mpango huo na linatoa onyo Kali kuwa wale wote wanaopanga na ambao watajaribu kutekeleza kinachohamasishwa watashughulikiwa vikali lakini Kwa mujibu wa Sheria za nchi

/ Published posts: 1975

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram